JANGA ALILOLIPATA BEKI WA ARSENAL

 ARSENAL

ARSENAL imejikuta katika hali tata kuelekea pambano lao la North London derby, baada ya beki wao tegemeo, Gabriel Magalhães, kushindwa kumaliza mchezo wa kimataifa kati ya Brazil na Senegal.

Nyota huyo wa ulinzi, ambaye amekuwa nguzo muhimu kwenye safu ya nyuma ya Arteta, alionekana kutokuwa katika hali nzuri wakati mchezo ukiendelea, na baadaye akatoa ishara kwa benchi la ufundi kabla ya kuomba kutolewa.

Gabriel mwenye umri wa miaka 27, aliachwa nje kipindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na Wesley, hatua iliyowaacha makocha wa Brazil wakiwa na wasiwasi, huku mashabiki wa Arsenal wakipatwa na taharuki juu ya hali yake.



Post a Comment

Previous Post Next Post