ARGENTINA KUSHIRIKIANA NA FIFA
π¨Mwandishi wa habari Romain Molina ametoa madai kadhaa yanayoihusisha FIFA na Chama cha Soka cha Argentina.π¦π·π₯΄ • Inadaiwa FIFA ilifunga uchunguzi dhidi ya kocha wa zamani wa timu ya vijana ya wanawake ya Argentina Diego Guachi baada ya kudaiwa kwa makosa ya unyanyasaji wa kijinsia kutoka kwa wachezaji watano na kesi hiyo FIFA Waliipuuzia. • Inadaiwa FIFA ilituma pesa za zawadi kwa Argentina baada ya kushinda Kombe la Dunia 2022 kwa kampuni yenye makao yake Miami badala ya AFA. Kampuni hiyo ambayo ipo chini ya uchunguzi wa FBI kwa madai ya ulaghai na utakatishaji fedha • Molina anadai maafisa wakuu wa FIFA wana uhusiano wa karibu na viongozi wa soka wa Amerika Kusini, na hivyo kuipa CONMEBOL ushawishi mkubwa katika miaka ya hivi karibuni. • Pia Molina Anadai kuna utamaduni wa kutokujali baadhi ya maafisa wa soka wa Amerika Kusini kufuatia kashfa za FIFA. • Kufuatia madai hayo Wabunge wa Bunge la Ulaya wametaka uchunguzi wa haraka dhidi ya rais wa FIFA Gianni Infantino.