TAARIFA KAMILI KWA MSEMAJI WA DAR YOUNG AFRICANS

 ALIKAMWE AKIZUNGUMZIA MECHI IJAYO DHIDI YA FARABAT



“Yanga SC itaelekea Zanzibar hapo kesho kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya FAR Rabat. Timu itaondoka saa tatu asubuhi kwa njia ya boti. Baadhi ya wachezaji kama Prince Dube, Celestine Ecua, Lassine Kouma waliokuwa bado kwenye majukumu ya timu zao za taifa hawatakuwepo kwenye safari hii ya kesho Lakini tayari uongozi umeshaweka taratibu zote vizuri ili wachezaji hawa wasafiri na kuungana na timu Zanzibar moja kwa moja.


“Wachezaji waliokuwa kwenye timu ya Tanzania wamesharejea na ni sehemu ya safari ya kesho. Niwaombe Wazanzibar kujitokeza kwa wingi kuipokea timu kesho na kuwaonyesha wachezaji wetu ni kwa kiasi gani mko tayari kwa ajili ya mchezo huu mkubwa wa Kihistoria. Zinakwenda kukutana timu mbili bora Afrika kwa sasa”. 

“Jezi mpya za Yanga kwa ajili ya msimu wa Ligi ya Mabingwa zitazinduliwa na kuanza kuuzwa siku ya Alhamisi. Nawakumbusha kuwa jezi hizi ni maalumu kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa hivyo mzigo hautakuwa mkubwa sana, Hivyo wananchi wanapaswa kuhakikisha wanajipatia jezi zao mapema. Binafsi nimeziona hizi jezi. Jambo la uhakika na ninalisema kwa kujiamini, jezi za kimataifa za msimu ni jezi za viwango vya juu sana” 

“Mechi ya Yanga dhidi ya FAR Rabat ndio mechi kubwa zaidi kuwahi kuchezwa katika uwanja wa New Aman Complex. Huu ndio mchezo unaozungumzwa zaidi barani Afrika kwa sasa. Usiifananishe mechi hii na mechi nyingine yoyote ambayo imewahi kucheza Aman Complex. Hakuna mtu anatamani kusimuliwa mchezo huu. Kila mtu anatamani kuwa New Aman Complex.


” Hakikisha unapata Tiketi yako mapema, zimeshaanza kuuzwa Leo kwenye vituo mbalimbali na kwa njia ya mtandao. 


“Kwa ambao mko Zanzibar, kadi zenu mtatumia zilezile, kama ulipoteza, kesho pale nje ya uwanja wa New Amaan Complex kadi zitakuwepo, njoo mapema nunua tiketi yako mapema usikose burudani hii kubwa Afrika.” 

“Tunaomba tuachwe tufanye kazi sasa. Muda wa kupiga maneno umeisha ni muda wa vitendo. Tunaposema tunakwenda kupambana na FAR Rabat kupata pointi 3 kwenye kundi letu, tunamanisha kweli mapambano. 


“Tumesikia kila neno ambalo mmeongea dhidi yetu. Tunahitaji kuwajibu kwa vitendo sasa. Maswali yenu yote tutawapa majibu sahihi. Mtakwenda kuishuhudia Yanga tofauti kabisa. 

“Kila mwanayanga ajiandae na kazi hii kubwa mbele yetu, usikubali kufumba jicho, usikubali kurelax, hii ni wiki ya kazi, tufanye maandalizi ya kazi kweli tukija uwanja wa New Amaan Complex Jumamosi” Meneja Habari ALLY KAMWE



Post a Comment

Previous Post Next Post