JAMBO KUU KUHUSU WIMBO WA TAIFA WA HISPAIN
Uliwahi kujiuliza kwa nini wachezaji wa timu ya taifa ya Hispania huwa hawaimbi wimbo wao wa taifa kabla ya mechi? Jibu ni rahisi: wimbo wa taifa wa Hispania, unaoitwa “Marcha Real” hauna maneno rasmi. Tofauti na nyimbo nyingi za mataifa mengine, huu ni wimbo wa ala pekee.
Ndiyo maana utaona wachezaji wakiwa wamesimama kwa heshima, lakini bila kuimba. Kumewahi kuwa na majaribio ya kutunga maneno, lakini hayakuwahi kukubaliwa rasmi. Hivyo, si kwamba wachezaji hawana uzalendo; hawana maneno ya kuimba. “Marcha Real” ni miongoni mwa nyimbo chache za taifa duniani zisizo na mashairi rasmi. Hii ndiyo siri ambayo wengi hawaijui kabisa.

Comments
Post a Comment