Posts

Showing posts from July, 2026

ARGENTINA KUSHIRIKIANA NA FIFA

Image
 🚨Mwandishi wa habari Romain Molina ametoa madai kadhaa yanayoihusisha FIFA na Chama cha Soka cha Argentina.🇦🇷🥴 • Inadaiwa FIFA ilifunga uchunguzi dhidi ya kocha wa zamani wa timu ya vijana ya wanawake ya Argentina Diego Guachi baada ya kudaiwa kwa makosa ya unyanyasaji wa kijinsia kutoka kwa wachezaji watano na kesi hiyo FIFA Waliipuuzia.  • Inadaiwa FIFA ilituma pesa za zawadi kwa Argentina baada ya kushinda Kombe la Dunia 2022 kwa kampuni yenye makao yake Miami badala ya AFA. Kampuni hiyo ambayo ipo chini ya uchunguzi wa FBI kwa madai ya ulaghai na utakatishaji fedha • Molina anadai maafisa wakuu wa FIFA wana uhusiano wa karibu na viongozi wa soka wa Amerika Kusini, na hivyo kuipa CONMEBOL ushawishi mkubwa katika miaka ya hivi karibuni. • Pia Molina Anadai kuna utamaduni wa kutokujali baadhi ya maafisa wa soka wa Amerika Kusini kufuatia kashfa za FIFA. • Kufuatia madai hayo Wabunge wa Bunge la Ulaya wametaka uchunguzi wa haraka dhidi ya rais wa FIFA Gianni Infantino.

CHAGUO JIPYA LA KOCHA WA SIMBA

Image
 🚨 TETESI ZA USAJILI SIMBA SC🦁 Inaeleza kuwa Simba SC inamfuatilia saini ya mshambuliaji wa shekhukhune ya pale nchini Africa Kusini katika dirisha kubwa la usajili! 🇿🇦 ✈️🇹🇿 Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 , anasifika kwa: • Kasi kubwa akiwa na mpira • Uwezo wa kupiga chenga na kupenya pembeni • Kutengeneza nafasi na kutoa pasi za mwisho (assists) • Kucheza kama Left Winger, lakini pia anaweza kucheza Right Winger na Centre Forward Je, unadhani atakuwa nyongeza sahihi kwa Simba SC? 🤔👇

THIBAUT KUJIONDOA KWA MUDA

Image
 Thibaut Courtois ametangaza nia yake ya KUJIONDOA KWA MUDA katika timu ya taifa ya Ubelgiji na kupumzika baada ya Ubelgiji kuondolewa kwenye Kombe la Dunia na Hispania. 👋🏻🇧🇪 🗣️ Courtois: “Nataka kupumzika kwa mwaka mmoja bila kucheza mechi yoyote ya Ubelgiji, kisha nirejee kwa mechi za kufuzu EURO pamoja na michuano ya EURO 2028. Sijui kama Shirikisho la Soka la Ubelgiji litakubali ombi hili.” Unadhani ni uamuzi sahihi?

JAMBO KUU KUHUSU WIMBO WA TAIFA WA HISPAIN

Image
 Uliwahi kujiuliza kwa nini wachezaji wa timu ya taifa ya Hispania huwa hawaimbi wimbo wao wa taifa kabla ya mechi? Jibu ni rahisi: wimbo wa taifa wa Hispania, unaoitwa “Marcha Real” hauna maneno rasmi. Tofauti na nyimbo nyingi za mataifa mengine, huu ni wimbo wa ala pekee.  Ndiyo maana utaona wachezaji wakiwa wamesimama kwa heshima, lakini bila kuimba. Kumewahi kuwa na majaribio ya kutunga maneno, lakini hayakuwahi kukubaliwa rasmi. Hivyo, si kwamba wachezaji hawana uzalendo; hawana maneno ya kuimba. “Marcha Real” ni miongoni mwa nyimbo chache za taifa duniani zisizo na mashairi rasmi. Hii ndiyo siri ambayo wengi hawaijui kabisa.

MISRI YAISHUTUMU ARGENTINA

Image
 ⚠️ MISRI WAISHUTUMU ARGENTINA! 🫵🤯 Kocha wa Misri, Hossam Hassan, amedai kuwa maslahi ya kifedha ndiyo yaliyoiwezesha Argentina kuendelea kwenye mashindano. 🗣️ "Yote yanahusu fedha. Wanataka Messi aendelee kubaki kwenye mashindano. Kwenye soka, mambo mengi hutokea nje ya uwanja kutokana na maslahi." 💬 "Kilichotokea hakikuwa cha haki. Misri ilistahili kufuzu. Tulikuwa timu bora dhidi ya Argentina."